The House of Favourite Newspapers

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi Aichambua Pacha ya Mayele, Musonda

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema anatarajia matunda mazuri kutoka kwa washambuliaji wake wawili, Kennedy Musonda na Fiston Mayele kutokana maelawano yao ya haraka licha ya kutowahi kucheza pamoja.

Mayele na Musonda ambao ni washambuliaji wa kati, Jumatatu ya wiki hii kwa mara ya kwanza walicheza pamoja katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu ambao Yanga ilishinda 1-0, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema kwa kiasi kikubwa anaamini wachezaji hao watakuwa na msaada mkubwa ndani ya Yanga kwa siku zijazo kutokana na kuelewana haraka zaidi jambo ambalo ni zuri.

“Unapokuwa na washambuliaji wazuri ni furaha kubwa sana kwa mwalimu, kwa Musonda na Mayele kuna muunganiko mzuri umeonekana haraka zaidi japo hawajacheza kwa pamoja na hawakuwahi kucheza pamoja huko nyuma.

“Kuna mechi nyingine zinahitaji kuwatumia washambuliaji wote wawili kwa pamoja watumike katika kikosi au kuanza kwa pamoja, hivyo unapokuwa na washambuliaji wanaoelewana ni jambo zuri kwa kuwa ndiyo kitu kinachohitaji kuonekana ili kilete faida kwenye timu,” alisema kocha huyo.

STORI: MARCO MZUMBE

KIMENUKA, CHAMA ATOA TAMKO SIMBA, BEKI MPYA YANGA KUTUA LEO…. | KROSI DONGO

Leave A Reply