The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Kocha Mkwasa wa Ruvu Shooting Ajiuzulu, Atoa Fursa kwa Viongozi Kutafuta Mbadala Wake

0
Kocha wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu kuifundisha timu hiyo

KOCHA MKUU wa Klabu ya Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu kuifundisha timu hiyo kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Akizungumza na Mtangazaji Maulid Kitenge wa EFM, Mkwasa amesema kuwa amefikia uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa watu wengine waende wakaendeleze pale ambapo ameishia huku akiiacha timu hiyo kwenye nafasi ya 15 ya msimamo ambayo ni ya pili kutoka mwisho.

 

Hadi sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC klabu ya Ruvu Shooting imekusanya jumla ya alama 11 baada ya kushinda michezo 3 na kutoka sare mara 2 katika jumla ya michezo 15 iliyokuwa imekwisha kuchezwa na klabu hiyo mpaka sasa huku ikiwa imepoteza jumla ya michezo 10.

Mkwasa ametoa fursa kwa viongozi wa Ruvu Shooting kutafuta mbadala wake

Ruvu Shooting imepoteza michezo minne mfululizo huku mara ya mwisho kwa klabu hiyo kupata ushindi ilikuwa ni Septemba 26, 2022.

“Nafikiri nimejiuzulu mpaka sasa hivi navyoongea na wewe, pengine inawezekana Philosopy yangu haieleweki vizuri kwahiyo naona ni vyema nikatoa fursa kwa viongozi kutafuta mtu mwingine. Alisema Mkwasa wakati akihojiana na mwandishi wa EFM Maulid Kitenge.

Leave A Reply