The House of Favourite Newspapers

Kocha mpya Simba amkataa Kerr

0

kochaDylanKerr.jpg
Hans Mloli na Sweetbert Lukonge
SIMBA inashinda mechi zake za Ligi Kuu Bara, lakini uongozi hauridhishwi na uwezo wa wachezaji, hivyo imepanga kumrejesha kocha wa viungo, Dusan Momcilovic.

Uamuzi huo umekuja baada ya kubainika kwamba, kila ikifika dakika ya 60 ya mechi zake, wachezaji huchoka na kupoteza stamina, hivyo kutoa nafasi ya wapinzani kucheza watakavyo.
Ndipo uongozi chini ya Rais, Evans Aveva ulipoona kuna haja ya kumrejesha Dusan ili aendelee na kazi yake ya kutengeneza stamina za wachezaji kama alivyofanya siku chache kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi.
Dusan amesikia mpango huo wa Simba, lakini akasema: “Naweza kurejea Simba kwani jambo muhimu ni kuipa timu ubingwa lakini sipo tayari kufanya kazi na Kerr, siwezi kufafanua zaidi.”
Hata Kerr naye alipoulizwa kama yupo tayari kufanya kazi na Dusan, alisema: “Kama watamrudisha basi watafute timu nyingine ya kumpeleka kwani hana nidhamu na anaweza kuiharibu timu yangu.”
Kabla hajaondoka nchini, Dusan aliweka wazi kutoelewana na Kerr ambaye anadai alichangia kwa kiasi kikubwa asiongezewe mkataba wake wa kazi ya ukocha wa viungo katika timu hiyo.

Leave A Reply