The House of Favourite Newspapers

Kocha Mpya wa Barcelona Huyu Hapa…

Mara baada ya Luis Enrique kutangaza kuwa ataondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu, taarifa za makocha watakaochukua nafasi yake zimekuwa zikizungumzwa kila kukicha.

Taarifa kutoka Barcelona zinaeleza kuwa mtu sahihi ambaye anapewa nafasi kubwa kuchukua mikoba hiyo ni Carlos Unzue ambaye ni msaidizi wa Enrique.

Sifa nyingi ziliongezeka kwa msaidizi huyo kutokana na jinsi alivyokuwa akiinuka kuhamasisha wenzake katika mchezo dhidi ya PSG na kutoa maelekezo kiasi kwamba Barcelona ikashinda mabao 6-1.

“Alikuwa na sisi miaka ya nyuma, akaondoka na kisha akarejea, anaonyesha yupo tayari kuwa kocha mkuu,” alisema nahodha wa Barcelona, Andres Iniesta alipomzungumzia kocha huyo.

Mbali na Iniesta ambaye ni mchezaji mkongwe klabuni hapo, pia amekuwa akiungwa mkono na

wachezaji wengine wengi kikosini hapo.

Ikumbukwe kuwa kuna kipindi Enrique alitibuana na staa wa timu hiyo, Lionel Messi, msaidizi huyo ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kuweka mambo sawa na kuwapatanisha.

Unzue aliwahi kuwa mchezaji wa Barcelona mwaka 1988 hadi 1990, baadaye akarejea akiwa kocha wa makipa mwaka 2003 chini ya Frank Rijkaard, pia alifanya kazi chini ya Pep Guardiola. Aliondoka Barcelona mwaka 2010, alirejea mwaka 2014 akiwa msaidizi wa Enrique ambaye walikuwa naye pamoja Celta de Vigo.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Arsenal imetenga kitita cha pauni milioni 25 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Barcelona, Arda Turan baada ya kuwepo kwa tetesi za kuondoka kwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez kikosini hapo mwishoni mwa msimu huu.

Comments are closed.