The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kocha Mpya wa Yanga Aanza Kazi Kwa kichapo, Afunguka – Video

0


KOCHA mpya wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji, ameanza kazi kwa kichapo baada ya jana kushuhudia timu yake ikifungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

 

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kwanza kwa Mbelgiji huyo tangu akabidhiwe mikoba hivi karibuni, ilishuhudia Yanga ikimaliza ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja baada ya kiungo wake, Mohammed Issa ‘Banka’ kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu dakika ya 44.

Katika mchezo huo, Yanga ilianza kwa kasi ikiwa chini ya nahodha, Haruna Niyonzima, lakini dakika ya 13, Yusuph Mhilu ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo, alifunga bao la kwanza kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Yanga, Farouk Shikalo.

 

Kipindi cha pili, Yanga ilijipanga kupindua meza lakini ikazidiwa mbinu na Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ambapo ikapata mabao mengine kupitia kwa Ally Ramadhani dakika ya 66 na Peter Mwalyanzi dakika ya 89.

Kichapo hicho cha Yanga kiliwakera mashabiki wa timu hiyo ambao muda mwingi walionekana kuwa na sura za huzuni, lakini wakajipa moyo kwamba wanaweza kukaa sawa katika mechi zijazo kutokana na kufanya usajili wa nguvu huku wakiwa na kocha mpya.

 

Hii ni mechi ya 13 kwa Yanga msimu huu ambapo timu hiyo imeweza kukusanya pointi 25, ikiachwa pointi 10 na Simba wanaoongoza ligi hiyo baada ya kucheza mechi 14.

 

Leave A Reply