Kocha Mpya Yanga Cedric Kaze Apewa Miaka Miwili

UONGOZI wa klabu ya Young SC leo Oktoba 16, 2020 umemtambulisha rasmi kocha mpya wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze na kumpa mkataba wa miaka miwili hadi 2020/22 wenye kipengele cha kuongeza mkataba.
Kaimu Katibu Mkuu wa kilabu hiyo, Simon Patrick, amesema kandarasi hiyo inaanza rasmi leo na kinachosubiriwa sasa ni kibali tu cha kufanyia kazi.

Kaze baada ya kusaini mkataba huo amesema kitu anachotaka kufanya kwa sasa ni kurejesha ukubwa wa timu hiyo huku akiahidi kuonyesha vitendo zaidi uwanjani kuliko maneno.




