The House of Favourite Newspapers

Kocha Mpya Yanga Zimebaki Saa 24 Tu

0

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umepanga kukutana kesho Jumamosi tayari kujadili majina ya makocha watatu waliopendekezwa kuionoa timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara huku jina la aliyekuwa kocha wa zamani wa Harambe Stars, Sebastian Migne raia wa Ufaransa likipewa nafasi kubwa.

 

Yanga imechukua uamuzi huo baada ya kuwa na majina ya makocha wa tatu wa kigeni kwa ajili ya kurithi mikoba ya Mrundi, Cedric Kaze aliyetimuliwa kutokana na timu kupata matokeo ya sare za mfululizo.

 

Uongozi tayari una jina la aliyekuwa kocha wa Township Rollers ya Botswana, Nikola Kavazovic raia wa Serbia, Hubert Velud raia wa Ufaransa na Sebastian Migne.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Ijumaa limezipata zinasema kuwa, uongozi wa timu hiyo umepanga kukaa siku ya Jumamosi kwa ajili ya kupitisha jina la atakayekuwa kocha mkuu ndani ya kikosi hicho.

 

“Mchakato wa kocha unaenda vizuri na kwetu wala hakuna presha kwa kuwa tunahitaji kuwa na mwalimu mwenye uwezo mkubwa na kuweza kusaidia vyema na kocha wetu anayekaimu, Juma Mwambusi.

 

“Lakini uongozi umepanga kukaa siku ya Jumamosi kujua nani atakuwa kocha mkuu kati ya hao makocha wa tatu ingawa kwa sasa Migne ndiye anapewa nafasi kubwa zaidi huenda ndiyo akapitishwa kwa kuwa mazungumzo yake na viongozi yameenda vizuri zaid,” alisema mtoa taarifa.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Fredirick Mwakalebela ambaye alisema kwa sasa mchakato wa kumtafuta kocha mpya unaendelea na utakapokamilika wataweka wazi kila kitu bila ya kuficha chochote katika suala hilo.

STORI: MUSA MATEJA NA IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply