The House of Favourite Newspapers

Kocha Nabi Bado Yupo Yupo Sana Yanga Aongeza Mkataba wa Miaka Miwili

0
Rais wa Klabu ya Yanga Mhandisi Hers Saidi (Kushoto) akiwa na Kocha Nasreddine Nabi baada ya kuongeza mkataba.

Klabu ya Soka ya Yanga imethibitisha kocha wake Nasreddine Mohammed Nabi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia timu hiyo ya ‘Wananchi’ hadi mwaka 2024.

 

Licha ya Nabi kuhitaji ongezo zaidi la mshahara ambao wameafikiana, kingine ni mipango yake ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania.

 

Kila Kocha anapenda kufanikiwa na timu anayofundisha hata kama haipendi. Nabi anaamini anaweza kupata mafanikio aliyokosa alikopita, kama Yanga wanavyoamini pia juu yake hasa kufuatia kuimarishwa kwa kila idara ndani ya kikosi hicho msimu huu.

 

Nabi ameiongoza Yanga kutwaa mataji matatu mhimu msimu uliyopita baada ya Yanga kuwa na ukame wa makombe kwa miaka minne. Baada ya kusaini kandarasi hiyo, Nabi amesema; “Bado nipo nipo sana, Safi fresh.

 

Msimu uliopita  Nabi aliongoza Yanga kutwaa Ngao ya Jamii ubingwa wa ligi kuu ambao walimaliza bila kufungwa, kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation).

Leave A Reply