Kocha Simba Aipa Yanga Tahadhari kwa Zesco

JACKSON Mayanga, Kocha Mkuu wa KMC ambaye amewahi kuzinoa Simba, Coastal Union na Kagera Sugar, ameipa tahadhari mapema Yanga kabla ya kuwavaa Zesco United kwenye mchezo wa kimataifa.

 

Yanga itamenyana na Zesco Septemba 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kurudiana nao Septemba 26, mwaka huu nchini Zambia ikiwa ni mwendelezo wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayanja alisema kuwa mpira wa sasa umebadilika na siyo kama zamani, kazi kubwa kwa Yanga inapaswa kushinda mchezo wa kwanza.

 

“Wachezaji wakipata ushindi mchezo wa kwanza ule uwezo wa kupambana na akili inaongezeka, ila kama watapoteza ama kulazimisha sare kinachofuata ni presha kwenye mchezo wa marudio na inakuwa rahisi kupoteza.

 

“Kwenye michuano ya kimataifa mbinu kali na akili ndizo zinamaliza mchezo mapema kwa kuwa wao wanapeperusha bendera ya kimataifa basi wabadili namna ya kufikiria na kujifunza kwa walioshindwa, watapata hasira za kupambana,” alisema Mayanja.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment