Kocha Simba: Ajibu, Mkude Nendeni Yanga

KOCHA wa viungo wa Klabu ya Simba, Adel Zrane, raia wa Tunisia, ameweka wazi kuwa kama itatokea kukawa na ulazima wa viungo wao wawili wa klabu hiyo ambao ni; Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu kuondoka kikosini hapo, basi anatamani kuona wakisajiliwa na timu kubwa kama Yanga.

 

Mkude na Ajibu wanamaliza mikataba yao Simba mwishoni mwa msimu huu, na kumekuwa na taarifa kuwa wachezaji hao wanahitajika na mahasimu wa Simba, Yanga ambapo tayari inaelezwa wachezaji hao wamesaini mikataba ya awali.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Zrane alisema: “Nimekuwa nikisikia taarifa nyingi kuwahusu wachezaji wetu Ajibu na Mkude ambao wanatajwa kuwa kwenye uwezekano wa kujiunga na Yanga.

Unajua suala la usajili haliko kwenye mikono yetu, sisi tunatoa mapendekezo halafu ni uongozi na mchezaji husika ndiyo hufanya maamuzi.

 

“Mkude na Ajibu wote ni wachezaji wazuri, na kama itatokea kuwa kweli wanaondoka basi ningefurahi kuona wanakwenda timu kubwa kama Yanga, ili wazidi kukuza viwango vyao kupitia ushindani uliopo kwenye hizi timu kubwa.

 

“Kama kocha nisingependa kuona mchezaji yeyote anaondoka Simba, lakini kuna wakati unafika inawezekana kufanya hivyo kukawa na faida kwa Simba, hivyo nawatakia kila la kheri wale watakaoondoka, naamini watafanya vizuri huko waendako na inawezekana wakarejea tena Simba.”

Stori: Joel Thomas,Dar es SalaamTecno


Toa comment