Kartra

Kocha Simba Atoa Kauli “Mtakuja Machinjioni”

BIG Bosi wa Benchi la Ufundi la Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amebainisha wazi kwamba, hajali sana matokeo ambayo waliyapata jana kwenye mechi yao na Kaizer Chiefs kwa kuwa hesabu zake ni kuimaliza mechi hiyo nyumbani.

 

Gomes ameongeza kwamba, kwake matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mechi hiyo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika yapo katika uwanja wao wa nyumbani ambao wamekuwa na matokeo mazuri sana.

 

Jana Jumamosi, Simba walikuwa na kibarua cha kupambana na Kaizer Chiefs kwenye Dimba la FNB nchini Afrika Kusini.Simba kwenye Uwanja wa Mkapa chini ya Gomes msimu huu, imefanikiwa kuwachapa vigogo Al Ahly, AS Vita, El Merrikh na FC Platinum.

Kocha huyo amesema hesabu zake ni kwenye mechi hiyo ya marudiano na anafahamu wana asilimia kubwa ya kufanya vizuri kutokana na mwendo mzuri wakiwa hapo.

 

“Tuna mechi ya marudiano nyumbani, na hii ni muhimu sana kuweka matumaini kwa sababu tumekuwa tunafanya vizuri hapo.“Naamini hata mechi hii tutaendelea na hali ileile ambayo tunakuwa nayo kila tunapocheza katika uwanja wa nyumbani.

”Katika mchezo wa jana, Simba iliambulia kipigo cha kwanza kikubwa zaidi msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa 4-0.

 

Mabao ya Kaizer Chiefs yalifungwa na Erick Mathoho dakika ya 6, Samir Nurkovic alifunga mawili dakika ya 34 na 57, huku Leonardo Castro dakika ya 63 akihitimisha ushindi huo.Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Uwanja wa Mkapa, Dar, Mei 22, mwaka huu.

STORI: SAID ALLY, DAR


Toa comment