The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba si mtu mzuri, awafanyia umafia Waarabu

ILIZOELEKA katika mechi za nyumbani za Simba za Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems alikuwa akitumia mfumo wa 4-3-3 yaani akianza na ma­beki wanne, viungo watatu na washambuliaji watatu.

 

Mfumo huo ndiyo ulikuwa ukimwongoza kupata ushindi mnono katika mechi dhidi ya Mbabane Swallows ambapo walishinda mabao 4-1 la­kini pia dhidi ya Nkana FC ya Zambia ambayo walishinda mabao 3-1.

 

Lakini katika mechi ya juzi dhi­di ya JS Saoura iliyochezwa Uwan­ja wa Taifa, Dar, Aussems aliwafanyia kitu mbaya Waarabu hao ambao waliamini kwenye mchezo huo angetumia mfumo huo wa 4-3-3 ambao tayari wa­likuwa wamejipanga kukabil­iana nao.

 

Badala yake Aussems alionyesha ukomavu wa hali ya juu katika soka na akaamua kubadili mfumo na kutumia mfumo wa 4-4- 2 akianzisha mabeki wanne, viungo wanne na washambuliaji wawili, lakini pia katika dakika za lala salama alibadili tena mfumo na ku­tumia 4-5-1 yaani mabeki wanne, viungo watano na mshambuliaji mmoja.

 

Hali hiyo iliwa­vuruga Waarabu hao na kujikuta wakipoteana kwa kiwango kikubwa katika eneo la kiun­go ambalo katika mechi hiyo wakati akitumia mfumo wa 4-4-2 lilichezwa na Mghana, James Kotei, Jonas Mkude, Mzambia Claytous Chama pamoja na Hassan Dilunga.

 

Katika mfumo wa 4-4- 2 ambao Aussems alianza nao kwenye mechi alianza kwa kuwatumia mabaki Ni­cholaus Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid na Pascal Wawa, wakati washambuliaji waki­wa Emmanuel Okwi na John Bocco.

 

Baadaye alifanya ma­badiliko kwa kumtoa Bocco na nafasi yake ikachuku­liwa na Meddie Kagere, pia alimtoa Dilunga sehemu ya kiungo na kumuingiza Mzamiru Yassin.

 

Katika dakika za lala salama alipoamua kubadili mfumo na kutumia ule wa 4-5-1, alimtoa Okwi na ku­muingiza Shiza Kichuya am­baye ni kiungo na kuifanya timu hiyo icheze ikiwa na mabeki wanne, viungo wa­tano na mshambuliaji mmoja ambaye alikuwa ni Kagere pekee.

 

Akizungumza hali hiyo, Aussems alisema: “Lengo lilikuwa kupata ushindi kwa hiyo ndiyo maana nililaz­imika kubadili mfumo kutoka ule wa 4-3-3 kwa sababu niliamini wapinzani wetu wa­likuwa wameshaufanyia kazi ili waweze kutuzuia kirahisi.

 

“Hata hivyo niwapongeze vijana wangu kwa kazi kubwa waliyoifanya na tu­meweza kupata ushindi ka­tika mechi yetu ya kwanza na sasa sisi ndiyo tunaoon­goza kundi letu.”

 

SWEETBERT LUKONGE, Dar es Salaam

Comments are closed.