Kocha Stars: Tutawa Furahisha Watanzani

Kocha Mkuu  wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,Etienne Ndayiragijje akiwa na kocha msadizi Selemani Matola.

SELEMANI Matola, Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa watawafurahisha Watanzania keshokutwa Jumapili kwa kupata ushindi kwenye mchezo wa nyumbani dhidi ya Sudan.

 

Stars kwa sasa ina kibarua kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon 2020.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Matola alisema kuwa vijana wamepewa mbinu mpya zitakazowasaidia kupata matokeo chanya uwanjani.

 

“Wachezaji wote wanatambua kwamba Watanzania wanawatazama na wanahitaji matokeo jambo linalowapa msukumo wa kupambana ili kuleta furaha kwa taifa.

 

“Imani ni kubwa kwamba tutafanya vizuri ukizingatia kambi imeanza mapema na kila mchezaji analitambua jukumu lake, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao,” alisema Matola.


Loading...

Toa comment