The House of Favourite Newspapers

Kocha Arsenal, Mchezaji Chelsea Wakutwa na Corona

0
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amekutwa na virusi vya ugonjwa wa Corona na mechi kati ya timu yake na Brighton iliyotarajiwa kuchezwa wikiendi imeahirishwa.

The Gunners wamefunga uwanja wao wa mazoezi na wafanyakazi wa klabu hiyo ambao waligusana na Arteta wamelazimika kujiweka karantini.

Ligi ya Premier itafanya mkutano wa dharura na klabu zote siku ya Ijumaa ili kuzungumzia kuhusu mechi zinazotarajiwa kuchezwa.

Mchezaji wa Chelsea, Callum Hudson Odoi.

”Hii kwa kweli inasikitisha”,  alisema Arteta, raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 37.

”Niliamua kupimwa baada ya kujihisi vibaya lakini nitarudi kazini mara tu nitakaporuhusiwa kufanya hivyo”.

Wakati huohuo mchezaji wa Chelsea, Callum Hudson Odoi, pia amepatikana na virusi vya Corona .

”Wachezaji wote wa Chelsea waliogusana naye kikiwemo kikosi chote cha wachezaji 11, wafanyakazi  na wakufunzi sasa watahitajika kujiweka karantini kwa kipindi cha siku 14,”  ilisema klabu hiyo ya ligi kuu nchini humo.

Licha ya kupatikana na ugonjwa huo, Callum anaendelea vyema na anatarajiwa kurudi katika uwanja wa mazoezi atakaporuhusiwa, ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Leave A Reply