The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kocha wa Simba Akimbilia TFF

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ni kama ameshtukia kitu baada ya kuliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwapa muda wa wiki mbili zaidi kujiandaa endapo Ligi Kuu Bara itakaporejea.

 

Kocha huyo ameomba muda huo kuwaweka vizuri wachezaji wake ili wasiukose ubingwa wa ligi msimu huu ambapo wakishinda mechi tano tu kati ya kumi walizonazo wanauchukua.

 

Hivi karibuni TFF ilitangaza kusogeza mbele ligi iliyopangwa kuendelea Mei 30, ambapo sasa itaendelea Juni 30, mwaka huu endapo kama maambukizi ya Virusi vya Corona yatapungua. Simba inayoongoza ligi ikiwa na pointi 71, tayari baadhi ya wachezaji wake wa kimataifa wapo majumbani kwao na mipaka imezuiliwa ambao ni Francis Kahata (Kenya), Sharraf Eldin Shiboub (Sudan), Meddie Kagere (Rwanda) na Clatous Chama (Zambia).

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Sven alisema kuwa ni ngumu kwa muda mfupi kutengeneza muunganiko wa wachezaji kucheza pamoja kama ilivyokuwa awali, hiyo ni kutokana na kutofanya mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu.

Sven alisema kuwa wiki hizo mbili alizo ziomba zinam tosha yeye na makocha wa timu nyingine kuziandaa timu zao na kuleta ushindani kama uliyokuwepo awali.

 

Aliongeza kuwa bado anaendelea kuwasisitiza wachezaji wake kufanya mazoezi kuendana na program aliyompatia kila mchezaji ili ligi itakapoanza wote wawe tayari kupambana. “Nisingependa kuliingilia shirikisho kwa hivi sasa, lakini ningependa kutoa maoni kama kocha kuwaomba muda wa wiki mbili za kuiandaa timu kabla ya ligi kuendelea. “Kama unavyo fahamu timu haijakaa pamoja muda mrefu kutokana na ligi kusimama kupisha maambukizi ya Virusi

MANARA AMUONYA JERRY MURO – “AKINITAJA TU, NAMDHALILISHA, ATAVULIWA U – DC”

Leave A Reply