The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Simba Azitolea Macho Dk 120 Kusaka Nafasi ya pili Ligi Kuu

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefichua kuwa ameamua kuwarejesha mazoezi haraka wachezaji wake kutokana kukabiliwa na dakika 120 za kumaliza msimu ambao hawakuweza kupata chochote licha ya kuonyesha upinzani mkubwa.

Robertinho ametoa kauli hiyo ikiwa Simba imebakisha mchezo dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajia kupigwa Mei 24, mwaka huu kabla ya kumalizana na Coastal Union ya Tanga ambapo Simba inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na jumla ya pointi 67.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Robertinho alisema kuwa, anaimani mchezo huo utakaopigwa wiki ijayo ndiyo sababu zilizopelekea kurejea katika uwanja wa mazoezi kujipanga na mechi hizo.

“Tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa kuvuna pointi sita ili kumaliza heshima ligi na kuanza kujiandaa kwa msimu mpya,” alisema kocha huyo na kuongeza:

“Naamini wachezaji wangu watapambana na kufanikiwa kufanya vizuri katika michezo iliyobakia kwa lengo la kurudisha furaha kwa mashabiki wetu na kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao maana hakuna ambacho tumepata msimu huu,” alisema Robertinho.

Stori Na Ibrahim Mussa

MSANII wa HIPHOP BONGO AFARIKI, ALITAZAMA MECHI ya YANGA na DRIPU AKITAMANI KUONA FAINALI,MKE AELEZA

Leave A Reply