The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Ubelgiji Abwaga Manyanga, Ni Baada ya Timu Yake Kutolewa Kombe la Dunia

0
Kocha Roberto Martinez amejiuzulu kama Kocha wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji raia wa Hispania Roberto Martinez ameamua kuachia ngazi kwenye nafasi yake ya Kocha Mkuu wa Timu hiyo kufuatia kuondolewa kwenye mashindano ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

 

Ubelgiji imeondolewa katika mashindano hayo mara baada ya kupata matokeo ya sare ya 0-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Croatia.

 

Taarifa iliyotolewa na Chama cha Soka nchini Ubelgiji imebainisha kuwa inamshukuru Kocha Martinez kwa huduma yake ya kipindi cha miaka sita lakini kama Taasisi imesikitishwa kwa kuwaangusha wananchi na Taifa la Ubelgiji kutokana na namna timu yao ya taifa ilivyocheza nchini Qatar.

Ubelgiji imetolewa katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar

Ripoti ya kuwepo kwa majibizano pamoja na ugomvi miongoni mwa wachezaji inatajwa kuwa sehemu ya mambo yaliyoiathiri Ubelgiji katika mashindano hayo.

 

Kevin De Bruyne alinaswa na Kamera akijibizana na Jan Vertonghen na hatimaye De Bruyne kuibuka mbele ya waandishi wa Habari na kusema kuwa timu hiyo ilikuwa na wachezaji wengi wenye umri mkubwa ndiyo maana ilishindwa kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Leave A Reply