The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Yanga Atoa Maagizo Magumu Kwa Mayele

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema ni muhimu kwa wachezaji wake wote kuongeza umakini kwenye ushambuliaji katika mechi zote wanazocheza.

Timu hiyo imekusanya pointi 71, baada ya kucheza mechi 27, kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele mwenye mabao 16 na pasi moja ya bao.

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Ipo wazi kuwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Dodoma Jiji 0-2 Yanga, hivyo leo wataingia uwanjani kulinda rekodi huku Dodoma Jiji wakiwa na hesabu za kuvunja rekodi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nabi alisema kuwa kila idara ni muhimu kutimiza majukumu yake kwa umakini kupata mabao mengi kuongeza hali ya kujiamini.

“Kinachotupa ushindi kwenye mechi ni mabao hivyo ni muhimu kwa kila mchezaji kufanya hivyo kuanzia safu ya ushambuliaji pale wanapopata nafasi kuzitumia kwa umakini.

“Wapinzani wetu wanajipanga kupata matokeo mazuri kwetu nasi tunajitahidi kufanya vizuri kila mchezo kwa kuwa tunawaheshimu tunapokabiliana nao,” alisema Nabi.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

Leave A Reply