The House of Favourite Newspapers

KOCHA WA YANGA ATUA OFISI ZA GLOBAL GROUP, AWATAJA SIMBA

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera akitua ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar mapema leo

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera Machi 5, 2019 ametembelea katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori, jijini Dar ambapo amefunguka kuwa Simba wana nafasi kubwa ya kupenya kwenye hatua ya robo fainali kutokana na mwenendo wa kikosi hasa baada ya kuwatungua waarabu Al Ahly kwenye mchezo wa marudio bao 1-0.

Zahera akisaini kwenye kitabu cha wageni Global Group

Simba leo wameanza safariwakiwa na msafara wa wachezaji 20 kuwafuata JS Saoura nchini Algeria mchezo utakaochezwa Machi 9 mwaka huu.

“Naona sasa Simba imekuwa na makali, ina uwezo wa kupenya hatua ya robo fainali ukizingatia wameanza kujijenga kisaikolojia na wana cheza vizuri, endapo watacheza wakiwa ni timu nawaona wanafika hatua ya robo fainali aambapoitawasaidia kuongeza pointi kwaajili ya Taifa la Tanzania,” amesema Zahera.

Zahera akisalimiana na Meneja wa Global Group, Abdallah Mrisho ofisini kwake.

Simba wanashika nafasi ya pili kwenye kundi D wakiwa na pointi sita, wapinzani wao JS Saoura wapo nafasi ya tatu huku anayeburuza mkia ni AS Vita akiwa na pointi nne na kinara wao ni Al Ahly mwenye pointi saba.

Zahera akisalimiana na mhariri wa gazeti la Championi Jumatatu Ezekiel Kitula.
Zahera akisalimiana na mhariri wa gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph, kushoto ni mwandishi wa gazeti la Championi Wilbert Moland.
Zahera akiwa na wahariri wa magazeti pendwa, kuanzia kushoto ni Richard Manyota, Erick Evarist na Elvan Stambuli kuanzia kulia ni Sifael Paul, Andrew Carlos, Amran Kaima.
Zahera akiwa na waandishi wa gazeti la Championi pamoja na Chicharito wa Yanga aliyeshika gazeti.

(PICHA NA MUSA MATEJA | GPL)

Comments are closed.