The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Yanga Nasredine Nabi na Beki wa Simba Wafungiwa Michezo Mitatu na Faini

0

Kocha wa Yanga, Mohamed Nasredine Nabi amefungiwa michezo mitatu na faini ya 500,000 kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno Mwamuzi wa Kati na wa Akiba katika mchezo dhidi ya Ihefu.

Kamati ya TPLB imesema Nabi aliendelea kuwashambulia licha ya kuonywa kwa kadi ya njano.

Katika hatua nyingine mlinzi wa kushoto wa Simba SC, Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu na faini ya shillingi 500,000 kwa kosa la kuingia Uwanjani masaa 6 kabla ya mchezo dhidi Mbeya City na kumwaga vitu vyenye asili ya unga unga .

Adhabu imetolewa kufata kanuni ya 41:5 ( 5.5) ya Ligi Kuu ya udhibiti wachezaji.

Leave A Reply