The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya England, Sven Eriksonn Afariki Dunia

0

Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya England, Sven-Goran Eriksonn amefariki dunia asubuhi ya leo, Agosti 26, 2024 baada ya kusumbuliwa na saratani ya kongosho kwa muda mrefu.

Januari mwaka huu, Eriksonn alivunja ukimya na kutoa taarifa zilizoishtua dunia, kwamba madaktari wake walimweleza kwamba alikuwa na muda wa kuishu usiozidi mwaka mmoja kutokana na saratani iliyokuwa imefikia hatua ya mwisho, terminal.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa soka tangu kitambo, bila shaka utakuwa unakikumbuka kizazi cha dhahabu, golden generation cha Timu ya Soka ya Uingereza.
Hapa tunazungumzia kikosi kilichokuwa na wachezaji mahiri kama David Beckham, Steven Gerrard, Frank Lampard na wengine wengi.

Nyuma ya kizazi hiki cha dhahabu, ndipo alipokuwepo mwamba Sven-Goran Eriksonn ambaye ndiye aliyekuwa kocha wa timu hiyo, kuanzia mwaka 2001 na 2006, kipindi ambacho Timu ya Taifa ya England ilikuwa tishio kwelikweli.

Enzi za uhai wake, Eriksson alizifundisha timu nyingine kama IFK Gothenburg, Benfica, Roma, Fiorentina, Sampdoria, Lazio, Manchester City na Leicester City ambapo pia alikuwa kocha wa timu za taifa za Mexico, Ivory Coast na Ufilipino kabla ya baadaye kustaafu baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 40.

Leave A Reply