The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga amkataa beki wa Azam

0

UNAAMBIWA kuwa Kocha wa Yanga Nassredine Nabi ndiye alieukataa usajili wa beki wa Azam FC, Yakubu Mohamed ambaye hapo awali alikuwa anahitajika ndani ya uongozi wa timu hiyo.

 

Yakub Mohamed ni mmoja kati ya wachezaji wanne walitangazwa kuachwa na uongozi wa Azam FC juzi Jumamosi huku wachezaji wengine wakiwa ni Ally Niyonzima, Mozizi Mpiana na Obrey Chirwa.

 

Chanzo cha ndani ya Yanga kimeliambia Championi Jumatatu kuwa uongozi wa Yanga ulikuwa katika harakati za usajili wa beki huyo ambaye walifahamu kuwa hayupo kwenye mipango ya Azam FC, lakini baada ya kupeleka ripoti ya usajili kwa kocha Nabi akagomea usajili wa beki huyo chanzo kikiwa kushindwa kucheza kwa muda mrefu na kuwa na nidhamu isiyo ya kuridhisha.

 

“Uongozi wa Yanga ulikuwa katika mipango ya kumsajili Yakub Mohamed ambapo tayari walishafahamu kuwa hayupo kwenye mipango ya Azam FC ya msimu ujao lakini baada ya kumpa ripoti ya beki huyo kocha wa Yanga akapendekeza kutosajiliwa beki huyo chanzo kikiwa ni nidhamu na kutocheza kwa muda mrefu.

 

“Kocha Nabi anahitaji mchezaji ambaye ataenda kuwasaidia Yanga katika michuano ya kimataifa ambayo watashiriki msimu ujao,hivyo anaependa kuona usajili wa wachezaji waliopata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu akimini ndiyo watakuwa na msaada mkubwa kwao kwaajili ya msimu ujao,” kilisema chanzo hiko.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, juu ya usajili wa beki huyo ndani ya Yanga mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga Dominck Albinus alisema kuwa; “Kila kitu kuhusu usajili kipo chini ya kamati yetu na benchi la ufundi la Yanga na pindi yanapokuwa tayari ndio yanawekwa wazi, mara nyingi huwa hatazungumzii tetesi kwani ni mambo ambayo huwa hayajakamilika,” alisema kiongozi huyo.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply