KOCHA YANGA APATA KIBURI LIGI KUU BARA – VIDEO
MABAO 11 waliotupia mastraika wa Yanga kwenye mechi sita yamempa kiburi, Kocha Mkongomani Mwinyi Zahera.
“Ukiangalia kwenye mechi sita timu imefunga mabao 11 hakuna timu ligi ambayo imefanya hivyo kwenye mechi zao sita ambazo wamecheza.
“Hivyo washambuliaji wangu niseme ni bora kuliko wengine sababu hakuna aliyewafikia ila hawapaswi kuridhika bado wana safari ndefu na wanahitaji kupambana na kufanya kweli kwa kufunga mabao kwa kila mchezo ambao watacheza,” alisema Zahera.
STORI NA MARTHA MBOMA
Comments are closed.