The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga awalilia wake za wachezaji

KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa anawahurumia wake wa wachezaji wa kikosi hicho, kutokana na kukosa muda wa kukaa na waume zao ambao wanabanwa na majukumu ya klabu hiyo.

 

Zahera alisema kuwa, kubana kwa ratiba ya ligi, kunawanyima nafasi wachezaji wake ya kupumzika na familia zao, kwa kuwa muda wote wanakuwa wapo kambini.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Zahera alisema: “Nawaonea huruma sana wake wa wachezaji wangu, kwa sababu hawapati muda wa kukaa na waume zao ambao muda wote wapo kambini wakijiandaa na mechi.

 

“Ratiba siyo rafi ki kwetu, kwa sababu tulicheza na Alliance wiki iliyopita, tukapanda ndege na kwenda Mtwara kucheza na Ndanda siku ya tatu yake, kisha tukarudi tena Mwanza kucheza na African Lyon.

 

“Katika muda huo hakuna hata mchezaji mmoja aliyepata nafasi ya kwenda kwake, wote walikuwa kambini kujiandaa na mechi hizo, nafi kiri hii ratiba inatubana sana hadi tunakosa muda wa kupumzika,” alimaliza Zahera.

Comments are closed.