Kocha Yanga: Kakolanya Akirudi Yanga, Naondoka

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa ikiwa kipa aliyegomea kazi, Beno Kakolanya (pichani) atabaki kikosini humo basi yeye atafunga kila kilicho chake na kurejea kwao DR Congo.

Hivi karibuni Kakolanya aligoma kucheza akishinikiza alipwe fedha zake za usajili na mishahara ndipo arejee uwanjani.

 

Kitendo hicho kilimkera Zahera na kumuona kama msaliti kwani wapo wachezaji wengi wanaodai lakini waliendelea kucheza.

Viongozi wa Yanga, jana Jumamosi walikaa kikao na Zahera wakimuomba amsamehe Kakolanya ili arejee kambini lakini kocha huyo alishikilia msimamo wake kwamba hataki kumuona kikosini na kama akirejea basi yeye ataondoka na kurejea kwao.

 

“Viongozi na kocha Zahera walikuwa na kikao kizito kuhusu Kakolanya

ambaye ameonyesha nia ya kurejea kazini baada ya kupewa shilingi milioni mbili kutoka kwa mdau wa Yanga.

“Hata hivyo bado hali inaonekana kuwa ngumu kwani Zahera amekaza na anadai kama Kakolanya atarudi basi yeye atafunga kila kilicho chake na kurejea kwao.

 

“Anadai hii itawavunja moyo wachezaji wengine ambao walikuwa wanadai lakini hawakugoma kama yeye, anaogopa kutengeneza matabaka, ndani ya timu” kilisema chanzo makini.

 

Alipotafutwa Zahera alisema: “Hapa Yanga sio Beno apekee anadai fedha, wapo wengi kama kumi hawajalipwa fedha za usajili lakini bado wapo sasa wote wakigoma mambo yatakuwaje ni nani ambaye atacheza?

 

“Nikirudi kwa Beno hakuna ambaye alimfukuza Yanga alikataa kuja mazoezini na kuungana na timu kuweza kusafiri na timu sababu anadai fedha zake na ni mchezaji ambaye ana mkataba.”

Kwa upande wake Kakolanya alisema: “Nipo tayari kurudi kuitumikia Yanga.”

Loading...

Toa comment