The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga SC Amsifu Ngassa

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Mcongo, Mwinyi Zahera amesema kuwa mshambuliaji wake Mrisho Ngassa ataisaidia sana timu hiyo.

 

Ngassa ni mchezaji mpya kwenye kikosi cha Yanga ambayo amejiunga nayo hivi karibuni akitokea Ndanda FC, lakini ikumbukwe kuwa aliwahi kucheza Yanga awali, Simba na Azam FC.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera alisema kuwa kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi ya nguvu na anaamini mazoezi hayo yatawasaidia kufanya vizuri katika msimu ujao huku akisema kuwa Ngassa ataibeba sana timu hiyo.

 

“Kikosi kazi kinaendelea vizuri wachezaji wamefanya mazoezi ya nguvu sana na naamini kuwa watafanya vizuri kwenye ligi kuanzia Agosti 22.

 

“Pamoja na wachezajio wengine kuonyesha uwezo wa juu lakini Ngassa ni mchezaji mzuri na naamini kuwa ndiye ataisaidia sana timu kwenye safu ya ushambuliaji.

 

“Nimemuona kwa kipindi kifupi hapa ameonyesha uwezo mzuri na wa kuvutia nafi kiri kila mmoja ameona kazi yake,” alisema Zahera.

Ibrahim Mressy, Dar es Salaam

Comments are closed.