The House of Favourite Newspapers

Ukwepaji kodi kumuondoa Messi Barcelona au kumpeleka jela

0

10326470_710565715645350_254671663_nLionel Messi
messi

Messi na baba yake Jorge.

STAA wa soka duniani ambaye anayeichezea timu ya mabingwa wa La Liga 2014/2015, Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za ukwepaji wa kodi nchini humo.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Mapato Hispania, ilisema kuwa kama hatalipa kodi hiyo mapema iwezekananvyo, atapandishwa kizimbani au ataondoka nchini humo hivyo hatoweza kuichezea Barcelona kwa kile kinachodaiwa kuwa amekuwa akikwepa kulipa kodi.

Staa huyo ana nafasi ya kukata rufaa mahakama ya rufaa nchini humo.

Inadaiwa kuwa Messi na baba yake, Jorge wanadaiwa kodi ya kiasi cha euro milioni 4.1 sawa na bilioni 10.2 za Kitanzania ambazo  hawakulipa kati ya mwaka 2007 na 2009. Wote wamekanusha tuhuma hizo.

Kutokana na taarifa iliyoandikwa na mtandao mmoja wa Hispania, inaonesha kuwepo na njama zinazofanywa ili Messi aondoke nchini humo baada ya serikali kung’ang’ania kufuatilia sakata hilo. Mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na Mamlaka ya Mapato ya Hispania vimekuwa vikimtaja sana Messi na sakata hilo la ukwepaji kodi.

Mwanzoni mwa mwezi huu wakili wa serikali ya Hispania amekariririwa akisema kuwa, serikali imewapa Messi na baba yake miezi mitatu walipe kodi wanayodaiwa na serikali hiyo, la sivyo watapandishwa kizimbani na kufungwa jela kwa miezi 22 kila mmoja.

Messi amekuwa akiichezea Barcelona tangu akiwa na miaka 13 na mkataba wake utamalizika mwaka 2018 huku akiwa ni mmoja wa wachezaji waliyeipa mafanikio makubwa timu hiyo ikiwemo kunyakuwa mataji kibao likiwemo la La Liga 2014/2015.

Leave A Reply