Koffi Olomide Atua Nchini, Manara Ampokea – Video

MWANAMUZIKI nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo, Koffi Olomide leo Agosti 28, 2021 ametua nchini  kunogesha kilele cha Wiki ya Wananchi kitakazofanyika kesho Jumapili Agosti 29 katika Uwanja wa Mkapa.

 

Koffi amepokelewa na msemaji wa Yanga, Haji Manara na mashabiki wa timu hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

 

Yanga kupitia wadhamini wao GSM ndio waliomleta Koffi ambaye awali inadaiwa alikuwa aje katika kilele cha watani wao Simba katika Simba Day.701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment