Koffi Olomide Kuisimamisha Dar Leo
MAESTRO wa muziki wa Rhumba barani Afrika, Koffi Olomide au Mopao anatarajia kulisimamisha Jiji la Dar kwa shoo ya kibabe katika Tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Koffi aliwasili jana, Jumamosi na kufanya jiji kutikisika kidogo baada ya wale waliokuwa hawaamini kama atakuja, kumshuhudia laivu.
Mopao alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam ambapo Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisimamia shoo ya kumpokea.
Muda mfupi baada ya Mopao kutua, wachezaji wa Yanga na Simba waliokuwa wamebaki Morocco nao walitua.
Stori: Sifael Paul