The House of Favourite Newspapers

Koffi Olomide Mgeni Rasmi Bethidei ya Pedeshee Jack Pemba (+VIDEO)

0

Koffi-Olomide

PESA inaongea! Msanii nguli wa Bolingo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide ‘Mopao’ anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa (bethidei) ya pedeshee mwenye jina kubwa Bongo, Jack Pemba inayotarajiwa kufanyika Februari 3, 2017 nchini Uganda.

koffi-olomide-2Hii imethibitishwa na Koffi mwenyewe kupitia kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kikimuonesha  akiwahakikishia mashabiki wake kwamba atakuwepo kwenye bethidei hiyo.

koffi-olomide-bling-bling2Koffi Olomide ‘Mopao’.

Mopao anaonekana akiwa nyumbani kwake huku akionesha magari kadhaa ya kifahari na kumshukuru Jack Pemba kwa kile alichomfanyia ingawa hajaeleza wazi ni jambo gani amelifanya Jack Pemba kwa Mopao.

Jack-Pemba (1)Jack  Pemba

JACK PEMBA NI NANI?

Jack  Pemba ni kijana raia wa Kitanzania anayeishi nchini Uganda, ambaye aliibuka na kupata umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 2,000, baada ya kuwasili akitokea Uingereza, inakosemekana ana mke mzungu na watoto.

auntjackEnzi hiozo, Jack Pemba na Aunt Ezekiel.

Akiwa Bongo, Jack Pemba ambaye ni mkali kwa ‘totoz’ aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa Filamu Bongo, Aunt Ezekiel, ambaye kwa sasa amezaa na dansa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mose Iyobo lakini wakaachana miezi michache baada ya kutoelewana.

Jack Pemba ni maarufu miongoni mwa wanamuziki, kwani ni mmoja kati ya mapedeshee wanaofahamika kwa kutunza kiasi kikubwa cha fedha jukwaani, huku akizawadiwa kwa kuimbwa kwenye nyimbo.

Capture Jack Pemba alivyoosha gari lake jipya kwa mvinyo.

TUJIKUMBUSHE

Mwaka jana, Jack Pemba alifanya sherehe ‘bethidei’ ya kufuru wakati akisherekea kutimiza umri wa miaka 42, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, nje ya Mji Mkuu wa Uganda, Kampala.

Katika sherehe hizo, kiasi cha shilingi milioni 100 za Uganda ziliteketea, katika sherehe iliyohusisha wageni wapatao 100 ambapo keki kubwa ilikatwa huku waalikwa wakiburudishwa laivu na bendi ya muziki.

Capture 3Katika kile kinachoonekana kama kulibariki gari lake jipya, Range Rover Sport 2016, katika video nyingine, Jack Pemba alionekana akiliosha na mvinyo (Champagne) unaotajwa kuwa ni miongoni mwa mivinyo ghali huku akilifuta gari hilo kwa kutumia noti za dola ya Marekani.

Watu wameanza kujiuliza kwa kuwa ameshazoeleka kufanya kufuru kubwa kwenye sherehe mbalimbali, mwaka huu itakuwaje kwenye bethidei yake? Pia ni kiasi gani cha pesa amemlipa mwanamuziki ghali barani Afrika, Mopao Koffie, hadi akakubali kuwa Special Guest wa Birth Day Party yake? Tusubiri, muda utatuambia! Wenyewe wanasema, Time Will Tell!!!

Cheki Koffie Olomide Mupao Anavyomfagilia Jack Pemba

Leave A Reply