Koleta akesha akilia Beijing

MSANII wa kitambo kwenye tansia ya fil¬amu Bongo Coletha Raymond ‘Koleta’ ameeleza kuwa alikesha akilia alipokuwa Beijing nchini China wakati akifanya kazi huko kisa kikiwa ni kumkumbuka mtoto wake aliyemuacha Tanzania.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Koleta ambaye alipotea kidogo kwenye kuigiza, alisema alienda Beijing kwa ajili ya kufanya kazi ya kuingiza Sauti za Kiswahili kwenye tamthiliya za Kichina, lakini alimuacha mtoto wake akiwa na mwaka mmoja tu kitendo kilichosababisha kila akimkumbuka anaji-fungia na kulia.

“Jamani nilivyokuwa kule kwa mara ya kwanza ndio nimejua mtoto anauma maana kila nilipokuwa natoka kazini nilikuwa na¬jifungia ndani, nalia mpaka wenzangu wanakuja kunibembe¬leza na kunipa moyo, nilijitahidi mpaka nikazoea ila kwa shida sana kwa sababu tu ilikuwa ni kazi lakini mtoto anauma jamani,” alisema Koleta.

Toa comment