Koletha: Ubaguzi ni Ugonjwa Sugu Bongo Muvi

MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Koletha Raymond ameibuka na kusema ubaguzi ni ugonjwa sugu unaoitafuna tasnia ya filamu Bongo ‘Bongo Muvi’ na kamwe hauwezi kutibika.

 

Akipiga stori na Shusha Pumzi, Koletha alisema ndani ya Bongo Muvi kumejaa ubaguzi, roho mbaya na unafiki ndiyo maana hata zinapotokea fursa za maendeleo ya sanaa, wanaonekana wasanii walewale huku wenye sanaa yao wakisahaulika kwani wahusika hawaangalii kazi ya mtu, bali wanaangalia wanayoyajua wao.

 

“Ubaguzi umeshakuwa ni ugonjwa sugu, usiotibika ndani ya Bongo Muvi hivyo ni ngumu kuuondoa maana umeshaota mizizi, umezaa mpaka una vitukuu, watu wameshahubiri hadi wamechoka, hakuna mabadiliko kwa sababu wahubiri wa kupiga kelele kuhusu ubaguzi ndiyo wanaoongoza kwa ubaguzi hivyo sanaa hii haiwezi kurudi kama zamani tena,” alisema Koletha.


Loading...

Toa comment