testiingg
The House of Favourite Newspapers

Kolo Toure Mbioni Kuinoa Wigan Athletic, Yaya Naye Ahusishwa Kuwania Nafasi Hiyo

0
Kolo Toure amefanya kazi na Brendan Rodgers kwa miaka mitano sasa

MLINZI wa zamani wa klabu ya Arsenal, Manchester City pamoja na Liverpool Kolo Toure yupo mbinoni kuwa kocha mkuu wa klabu ya Wigan Athletic kufuatia klabu hiyo kumtimua kazi kocha wao Leam Richardson wiki iliyopita.

 

Toure (41) kwa sasa ni kocha msaidizi wa klabu ya Leicester City akiwa amefanikiwa kufanya kazi na kocha mkuu wa klabu hiyo Brendan Rodgers kwa kipindi cha miaka mitano (5) hadi sasa.

 

Taarifa zinasema kuwa Mabosi wa Wigan wamevutiwa na mipango ya Toure ambaye atakuwa na kibarua cha kuikwamua Wigan Athletic kutoka katika nafasi za hatari.

Leam Richardson Kocha aliyetimuliwa Wigan Athletic

Aidha mdogo wake na Kolo, Yaya Toure naye alikuwa akihusishwa na mpango wa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo lakini kwa sasa ataendelea na majukumu yake ya kuwanoa vijana waliopo katika kituo cha kulelea vipaji ndani ya klabu ya Totenham Hotspurs.

 

Naye Kocha aliyetimuliwa Leam Richardson ameandika taarifa kupitia ukurasa wake wa mkitandao ya kijamii akioneshwa kuhuzunishwa kutimuliwa katika nafasi hiyo.

Leave A Reply