The House of Favourite Newspapers

KOMBE LA DUNIA: URUSI YAINYUKA SAUDI ARABIA 5-0 (VIDEO)

MCHEZO wa ufunguzi wa michuano ya fainali ya Kombe la Dunia umemalizika Uwanja wa Luzhniki kwa wenyeji Urusi kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Waarabu, Saudi Arabia.

Mechi hiyo ya aina yake imeshuhudiwa bao la kwanza likiwekwa kimiani mnamo dakika ya 11 na Ganzizky ambalo limeandika rekodi ya kuwa bao la kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu.

Mabao mengine yametiwa kimiani na Cheryshev (43′, 90’+1), Dzyuba (71′ ) na Golovin (90’+4).

Baada ya wenyeji kuanza vizuri, mechi zingine za kesho zitakuwa ni Iran itakayowakaribisha Morocco na vilevile Ureno itakuwa inacheza dhidi ya Spain.

 

Highlights FIFA World Cup 2018: Russia vs Saudi Arabia

Comments are closed.