The House of Favourite Newspapers

Kombe la Shirikisho Afrika: Geita Gold Wapelekwa Sudan

0
Geita Gold FC

MATAJIRI wa madini, Klabu ya Geita Gold imepangwa kukutana na timu ya Hilal Al Sahil ya Sudan Kaskazini katika mechi ya hatua ya awali raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

 

Katika raundi ya pili ya mtoano, mshindi kati ya Geita Gold na Hilal Al Sahil atakutana na Pyramids FC ya Misri.

 

Mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 9, 10 na 11, mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano raundi ya kwanza zitapigwa Septemba 16, 17 na 18 mwaka huu.

 

Adha, michezo ya kwanza raundi ya pili ya mtoano itapigwa Oktoba 7, 8 na 9 mwaka huu 2022 wakati mechi za marudiano za raundi ya pili ya mtoano zitapigwa Oktoba 14, 14 na 16, mwaka huu.

Leave A Reply