The House of Favourite Newspapers

Kombinesheni 5 Hatari Yanga SC

0

YANGA kuelekea Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba itakayochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, tayari ina kombinesheni tano za hatari wanazor-inga nazo kwamba zina-wapa matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

 

Mashabiki wao wanatamba wakisema: “Hapa Mnyama hachomoki Jumamosi, lazima tuondoke na pointi tatu.

 

”Mabingwa hao wa kihistoria kwenye Ligi Kuu Bara, wana rekodi nzuri kwenye ligi hiyo msimu huu kwani hadi sasa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mechi baada ya kucheza mechi tisa.Yanga inayonolewa na Kocha Mrundi, Cedric Kaze, imeonekana kuwa bora kwenye mechi zake za hivi karibuni kiasi cha kutengeza kombinesheni hizo

 

MICHAEL SARPONG & DITRAM NCHIMBI

Nyota hawa wawili, pacha yao ilianza kujibu mchezo wa kwanza wakati Yanga ikiwa chini ya Zlatko Krmpotic ambapo ilicheza mchezo wa kirafi ki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi, bao la kwanza la Sarpong Bongo alifunga kwa pasi ya Nchimbi.Ilijibu tena kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United, Sarpong alifunga bao kwa pasi ya Nchimbi.

 

FARID MUSSA & WAZIR JUNIOR

Kiungo Farid pacha yake ilijibu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Yanga ikishinda mabao 2-1. Alipiga mpira wa kona uliounganishwa na Junior kwa kichwa.

 

MICHAEL SARPONG & WAZIR JUNIOR

Washambuliaji hawa wawili wamekuwa wakicheza kwa maelewano kwenye mechi mbili mfululizo chini ya Kaze. Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya KMC ambapo Sarpong alisababisha penalti kwenye ushindi wa 2-1 na mchezo wa pili walizidi kuwa karibu ni kwenye mchezo dhidi ya Biashara United ambapo Sarpong alifunga bao la ushindi.

 

TUISILA KISINDA & TONOMBE MUKOKO

Kisinda na Mukoko walikuwa pamoja ndani ya AS Vita na sasa maisha yao yanaendelea ndani ya Yanga. Pacha yao kwa mara ya kwanza ilijibu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba ambapo Mukoko alifunga bao kwa pasi ya Kisinda wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

 

BAKARI MWAMNYETO & LAMINE MORO

Miongoni mwa ukuta bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu ni huu unaoundwa na Bakari Mwamnyeto ambaye ni mzawa pamoja na Lamine Moro raia wa Ghana.

 

Kombinesheni yao kwenye mechi 9 ambazo ni sawa na dakika 810, wameshuhudia mabao mawili, bao la kwanza Mwamnyeto alicheza bila Lamine dhidi ya Prisons kwenye sare ya 1-1 na ni mechi moja walikuwa pamoja dhidi ya KMC wakati wakishinda 2-1.

 

Moro amekosekana kwenye mechi mbili akicheza mechi saba huku Mwamnyeto akikosa mechi moja dhidi ya Gwambina FC iliyomalizika kwa suluhu.Kaze ameliambia Spoti Xtra kuwa:

 

“Kwa wakati huu akili zote ni kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Simba, utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa ila sina mashaka katika hilo ninawaamini vijana wangu watafanya vizuri.”

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA | SPOTI XTRA | NOV 5, 2020

Leave A Reply