Kombinesheni ya Morrison, Bocco Simba hatari

MSHAMBULIAJI tegemeo ndani ya Simba, John Bocco na kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Mghana, Bernard Morrison, hadi sasa wametengeneza kombinesheni ya hatari katika kikosi hicho kwa msimu huu wa 2020/ 2021.

 

Morrison na Bocco tayari wakiwa wamecheza sambamba katika mechi tatu, wameonekana kuelewana zaidi na kwa pamoja kutikisa nyavu mara nne.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, tangu ampe Morrison nafasi kwenye kikosi cha kwanza, amekuwa akiendelea kumtumia na kuleta matunda kikosini hapo.

Katika mchezo wa kwanza ambao wawili hao walicheza pamoja, ilikuwa ni kwenye Simba Day dhidi ya Vital’O ambapo Simba ilishinda 6-0.Bocco alifunga bao moja lililotokana na asisti ya Morrison, huku Morrison naye akifunga bao moja.

 

Mechi ya pili ilikuwa ni ya Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo ambapo Morrison alifanyiwa faulo ndani ya eneo la hatari, ikawa penalti iliyofungwa na Bocco, kisha baadaye Morrison akafunga bao lingine, Simba ikashinda 2-0.Baada ya kucheza mechi hizo mbili, wawili hao pia wakaanza pamoja kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu iliyochezwa wikiendi iliyopita ambapo Simba ilishinda 2-1.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Bocco aliyepokea pasi ya Morrison, huku lingine likifungwa na Mzamiru Yassin.

 

Morrison katika kikosi cha Simba alichojiunga nacho msimu huu akitokea Yanga, anachezeshwa winga ya kulia na kushoto ambapo hapo awali ndani ya Simba walikuwa wakitumika Francis Kahata raia wa Kenya na Luis Miquissone kutoka Msumbiji.

 

Morrison akitokea pembeni anakuwa na kasi akiwa anakokota mpira akilitafuta eneo la ndani ya 18 huku akitengeneza nafasi za kufunga mabao huku nyingine akizutumia yeye kupachika mabaoTecno


Toa comment