The House of Favourite Newspapers

Kongamano La Biashara, Uwekezaji Kati ya Tanzania na Malawi Kufungua Biashara Zaidi

0
Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na  Ubalozi wa Tanzania-Malawi, Kituo cha Uwekezaji (TIC), Sekta Binafsi, TCCIA na TWCC imeratibu Kongamano la  Kibiashara kati ya Malawi na Tanzania lililofanyka kuanzia Tarehe 26 hadi 28 Aprili 2023 katika jiji la Mzuzu nchini Malawi.
Kongamano hili lilihudhuriwa na zaidi ya Wafanyabiashara 300 ambapo  Wafanyabiashara  150 ni wa Tanzania, wakingozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah aliyemwakilisha Mhe.Waziri Dkt. Ashatu Kijaji. Aidha Taasisi  na Idara mbalimbali mbalimbali zinazowezesha Biashara zilizoshiriki ni pamoja na TBS, TRA, Mamlaka ya Bandari, Uchukuzi, Shirika la la Meli, TMDA, Bodi ya Sukari , Tume ya Ushindani (FCC), ofisi za Wakuu wa Wilaya Ileje na Mbeya.
Kongamano hili lilishirikisha wafanyabiashara wa kati na pia  Kampuni kubwa za  teknolijia ya uongezaji thamani, viuatlilifu na zile za kifedha za Tanzania Ikiwemo Benki ya CRDB, Stanbic na pia Vodacom-Mpesa ili kuhakikisha masuala ya fedha na mawasiliano yanaendelea kuboreshwa na kuwezesha biashara zaidi.
Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Malawi Mhe. Simplex chithyola Banda, ameelekeza Kituo Cha Biashara Malawi kushirikiana na Tanzania kuandaa kongamano kila baada ya muda mfupi tofauti na kipindi cha Miaka mitano tangu lifanyike la Kongamano la kwanza upande wa Tanzania.
Mhe. Waziri Amewasisitiza Wafanyabiashara kutumia fursa na mahusuano mazuri kuboresha Biashara.
Naye Katibu Mkuu Dkt. Hashil Abdalah amewahakikishia wafanyabiashara kupata ushirikiano wa kutosha Kwa kuwa mazingira ya Biashara yameboreshwa na Taasisi zake zote ikiwemo TanTrade zipo tayari kutoa mwongozo na Taarifa za Biashara kuwezesha Mauzo ya Nje.
Kwa upande wa Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Cuba ambaye alikuwa akiwakikisha Tanzania nchini Malawi, Mhe. Balozi Humphrey Hezron Polepole amesema kongamano hilo limewakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika biashara zao baina ya nchi hizo.
Pia amewashauri watanzania kuwa wabunifu na kushirikiana na wafanyabiashara wa Malawi kutumia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Malawi ambayo ni moja ya nchi sisizokuwa na bahari. Tanzania na Malawi zimekubaliana kukuza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo ikiwemo uboreshaji wa sheria za uwekezaji, ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Kasumulo na huduma za Bandari ya Mbamba Bay ili kukuza biashara na uchumi katika nchi hizo.
Hayo yamesisitizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Aprili 26, 2023 alipokuwa akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
Aidha, amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Malawi kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania katika sekta za kilimo, uvuvi, uchumi wa bluu, uzalishaji utalii, huduma za fedha, uchukuzi, miundombinu, mawasiliano, madini elimu na afya ili kukuza biashara na uchumi wa nchi hizo.
Vilevile amewataka wafanyabishara na wawekezaji wa Tanzania kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana baina ya nchi hizo kulingana na rasilimali zilizopo katika nchi hizo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara ambayo imefikia kiasi cha dola za Marekani milioni 86.7 mwaka 2022.
Katika suala la uhusiano na Diplomasia, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, aliwasilisha shukrani kwa niaba ya Rais wa Malawi  Mhe. Lazarus Chakwera  ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Msaada wa chakula na vifaa vya kujihifadhi aliyoutoa wakati Malawi ilipokumbwa na kimbunga freddy mapema Machi 2023.
Tanzania na Malawi zimekubaliana kushirikiana katika kuboresha huduma za mpakani, huduma za kifedha na usafirishaji ili kuwarahisishia wafanyabiashara baina ya nchi hizo kufanya biashara kwa ufanisi na kukuza biashara zao na uchumi kwa ujumla.
Akifafanua kuhusu uboreshaji wa huduma za kifedha, Balozi Polepole amesema benki za Tanzania na Malawi zinapaswa kushirikiana na kuunganisha mifumo ili kuwawezesha wafanyabiashara kulipia bidhaa na huduma, ushuru wa forodha na tozo kwa urahisi bila kubadilisha sarafu katika nchi husika hali inayo poteza muda mwingi na gharama kubwa.
Kwa upande wa huduma za mipakani Mhe. Polepole amesema nchi hizo zimekubaliana kutekeleza makubaliano ya Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Pamoja (JPC) iliyokutana mwaka 2022 Dar es salaam kwa kukamilisha ujenzi wa vituo vya pamoja kwa mpaka wa Malawi na Kasumulo kwa mpaka wa Tanzania pamoja na kuongeza saa za kazi kutoka saa 12:00 jioni hadi saa 4:00 usiku kuanzia mwezi Julai, 2023. Aidha,  umuhimu wa kutumia ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor) pamoja na Bandari ya Mbamba Bay katika kusafirisha bidhaa mbalimbali kama saruji na mbolea ambayo ina uhitaji mkubwa nchini Malawi.
Akifafanua zaidi maelezo ya Mhe. Balozi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda ya Malawi Bi. Christina Zakeyo amesema Malawi iko tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Tanzania kwa kukamilisha orodha ya pamoja ya bidhaa(Simplified Trade Regime – STR) kwa Wafanyabiashara wadogo wanaovuka mpaka na mambo mengine ambayo Malawi itayashughulikia ni pamoja na kuhakikisha Mpaka wa Kasumulu / Songwe (OSBP) unaanza kufanya kazi; Kutatua changamoto za taasisi za Viwango; Utaratibu wa benki za Tanzania na Malawi (FDH na CRDB) ili zianze kubadilisha fedha moja kwa moja.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania walioshiriki maonesho katika Kongamano akiwemo Bw. Humoud Salim, (farmbase ltd) Bw. Daniel Malagashimba (sekta ya Utalii) na Bi Genovefa Barnabas (sekta ya kilimo) wamesema kongamano hilo limeleta manufaa makubwa katika kukuza biashara zao nchini Malawi kwani wameanza kupokea oda kubwa kupitia programu hiyo. Wafanyabiashara walioshiriki Maonesho ya kibiashara na Mikutano iliyoendeshwa sambamba na Kongamano wameweza kutengeneza fursa ya Biashara za moja kwa moja zaidi ya USD 100,000 kwa kuanzia.
Kama sehemu muhimu ya kuhitimisha Kongamano hilo,
TanTrade imeshrikiana na Taasisi ya Biashara Malawi (MTC) kuwatembeza Wafanyabiashara katika kiwanda cha Kwithu Kitchen na pia shamba la zao la Makademia (hekta 2000) la kampuni ya Tropha Mzuzu  kujifunza kwa vitendo kuhusu uzalishaji na uongezaji thamani pamoja na Biashara za Kimataifa.
Kufahamu taratibu za Mauzo ya Nje (exports) bofya:  trade.tanzania.go.tz
Leave A Reply