The House of Favourite Newspapers

Kongamano la USAGM/VOA 2022 Lilivyowakutanisha Viongozi wa Vyombo vya Habari Nchini Afrika Kusini

0

SHIRIKA la Habari la Sauti ya America (VOA) kwa kushirikiana na bodi ya Utangazaji ya Marekani (USAGM) na Shirika la Utangazaji la Global Press, wameendesha kongamano la namna bora ya kuimarisha vyombo vya habari kwa washirika wake wa barani Afrika.

 

Kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu katika Hoteli ya Kimataifa ya Pearl Valley, Cape Town, nchini Afrika Kusini, kuanzia Juni 24 – 26, 2022 likiwajumuisha washirika wa VOA kutoka nchi mbalimbali.

 

Viongozi wa washirika wote wa Sauti ya Amerika (VOA) kutoka vyombo vya habari vya Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Sudani Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Ethiopia, Seychelles na DRC wamehudhuria na kujifunza mbinu na kanuni mbalimbali za kutumia katika mazingira mbalimbali, bila kuhatarisha maisha ya waandishi wake.

 

Wakuu wa Kanda za VOA, kutoka kushoto na kanda zao kwenye mabano; ChuoChuo (DR Congo), Mack (Afrika Kusini) Joyce (South Afrika), Travis (Marekani), Salwa (Marekani), Koome (Kenya) na Rebecca (Afrika Kusini). Kongamano la mwaka huu lilifanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Pearl Valley, Cape Town, nchini Afrika Kusini, Juni 24 – 26, 2022.

 

Washirika wa Sauti ya Amerika (VOA) barani afrika, kutoka kushoto waliokaa na nchi walizotoka kwenye mabano; Davies Kabuswe (Zambia), Jacqueline Mwakyambiki (Tanzania), Farther David Niwagaba, (Malawi). – Waliosimama kutoka kushoto – Grey Phiri (Malawi), Orlando Muye (Kenya), Zweli Sibanda (Zimbabwe) na Nasser Hussein (Somalia)

Hawa walisherehekea ‘Birthdays’ zao wakati wa Kongamano, Juni 26, 2022. Kutoka kushoto Peter Mbungoma (Zambia), Nsinazo Warrakah (Kenya), Fred Afune (Kenya), Maurice Mugisha (Uganda) na Teacher Don Wanyama (Uganda).

 

Washirika wa Sauti ya Amerika (VOA) barani Afrika, kutoka kushoto; Hafidh (Zanzibar), Nasra Omar (Somalia), Costa (Zambia), Peter Mungoma (Uganda), Nsinazo Warrakah (Kenya), Abdallah Mrisho (Tanzania) na Berard Dupres (Seychelles).

 

Washirika wa Sauti ya Amerika (VOA) barani Afrika, kutoka kushoto; Fred Afune (Kenya), Mary Ayiik (South Sudan), Steve Diallo (Tanzania), Modesta Mselewa (Tanzania), Chris Ngong (Sudan) na Maurice Mugisha (Uganda).

 

Mkufunzi wa kongamano la VOA, Laxmi Parthasarathy kutoka Shirika la Habari la Kimataifa la Global Press la nchini Marekani, akitoa somo kwa washirika wa VOA.    (PICHA  ZOTE NA CHARLIE JAY)
Leave A Reply