The House of Favourite Newspapers

KONKI MASTER ALAINIKA KWA GIGY MONEY

AMA kweli hakuna mkate mgumu mbele ya kikombe cha chai ya rangi! Ndivyo ilivyo kwa mahaba kwani ukipatikana ni lazima ulainike kama Delila alivyomlainisha Samson katika Kitabu cha Biblia.  Hivyo ndivyo ilivyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva aliyewahi kuvuma kwa ubabe, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ au ‘Konki Konki Konki Master’ kunaswa akiwa mdogooo, akijichekea tu alipowekwa kwenye himaya ya kimahaba ya msanii mwenye makeke lukuki, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

Wawili hao walinaswa nyuma ya jukwaa la Wasafi Festival katika tamasha lililofanyika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Halmashauri ya Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa mbapo Gigy alikuwa ameshapanda jukwaani na kuwapa burudani wakazi wa eneo hilo. Katika tukio hilo, wawili hao walinaswa wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba huku kila mmoja akionekana kukolea kwa mwenzake.
Licha ya Konki Master kusifika kwa ugumu, lakini katika tukio hilo alionekana akiwa ndembendembe kwa mdada huyo, hali iliyozua minong’ono na kusababisha wapiga chabo kuanza kuwajadili. “Jamani yule Konki Master na Gigy aliyeimba Papa kumbe ni mtu na naniliu wake kha..!” Alisikika mmoja wa wapiga chabo wa Sumbawanga.

Baada ya kuwapiga picha za kutosha, Risasi Mchanganyiko lilitaka kuwahoji wawili hao ili kujua kama kuna jipya kati yao, lakini waliomba waachwe wapumzike kwa madai kwamba walikuwa wamechoka kuhojiwa, lakini kama kulikuwa na mtu hajui kusoma hata picha tu zenyewe zilikuwa zinatosha. “Hebu tuache bwana tupumzike…” alisema Gigy ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na jamaa aitwaye Moj

Stori: Richard Bukos 

Comments are closed.