The House of Favourite Newspapers

Kopa: Sina Stress ya Mwanaume!

0

MWANAMUZIKI mkongwe wa Taarabu, Khadija Omary Kopa amefunguka japo amepitia mtihani mkubwa wa kufiwa na mumewe, lakini mpaka sasa hana stress za mwanaume yeyote yule zaidi ya Mwenyezi Mungu.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Kopa alisema kuwa wanawake wengi wanakuwa na mawazo yaliyopitiliza kutokana na kuwawaza wanaume jinsi wanavyowaumiza kila kukicha, lakini kwa upande wake alishaachana na hizo habari.

“Yaani sijui niseme nini, sina stress za kumuwaza mwanaume yeyote hapa duniani, badala yake anayenipa stress ni Mungu tu kwa maana najitahidi kutenda yanayomfurahisha na si kitu kingine,” alisema Hadija Kopa

Leave A Reply