The House of Favourite Newspapers

Ubabe Wake wa Kijeshi, Korea Kaskazini Yafanya Magumashi ya Makombora

0
Maonyesho ya Kijeshi ya Korea Kaskazini yalionyeshwa kote duniani.

Pyongyang: Korea Kaskazini imelaumiwa kwa kuonyesha silaha bandia katika maonyesho ya hivi karibuni ya ubabe wake wa kijeshi.

Afisa wa zamani wa masuala ya ujasusi anasemna baadhi ya bunduki na makombora yaliyotumiwa kwenye maonyesho hayo yalikuwa bandia.

Maonyesho ya Kijeshi mjini Pyongyang

Michael Pregent alikiambia Kituo cha Runinga cha Fox kuwa baadhi ya bunduki zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilikuwa ni za bandia (magumashi). Lakini maonyesho kama hayo kuonyesha ubabe wa kijeshi yametumiwa kwa miongo kadhaa.

Mruka na mwavuli bandia wakati wa vita vya pili vya dunia

Kwa sasa msukosuko ni mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini. Hii ni baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kuapa kuwa ni lazima atakabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini.

Bunduki bandia za miti

===>“Sio kuwa Korea Kaskazini inafikiri kuwa itashinda Marekani lakini kile itafanya ikiwa itashambuliwa,” Pregent alisema.

Silaha hizi bandia zilitengenezwa kukwepa mashambulizi ya angani na kuwachanganya marubani ya jeshi kushambulia vifaru bandia baada ya vifaru halali

Wanajeshi wa Korea Kaskazini.

Wasanii wa jeshi la Ufaransa nao walichora mito bandia na mitaro ili kuwachanganya marubani wa ndege za vita. Ujanja kama huo pia ulitumiwa wakati wa vita vya pili vya Dunia

Vifaru bandia vilitumiwa na Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia kuonyesha ubabe wa kijeshi

Miti hii ilipakwa rangi hadi kifanana na silaha ya kurusha makombora. Lengo lilikuwa ni kuwachanganya maadui kuhusu ni wapi kulikuwa na adui. Aina hii ya silaha bandia zilitumika karne za 18 na 19.

===>Picha hii inaonyesha wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia miaka ya 1920

Leave A Reply