Korea Kaskazini yajaribu bomu la haidrojeni, ni utabiri wa TB Joshua

prophet-tb-joshua Nabii T.B. Joshua.

SIKU tatu baada ya Nabii T.B. Joshua wa Nigeria kuonya kuongezeka kwa nguvu za kijeshi za Korea Kaskazini, nchi hiyo iliyo chini ya utawala wa Kikomunist, imejaribia kwa mafanikio bomu la haidrojeni.

Joshua alikuwa ametoa wito wa kumwombea kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un, katika ujumbe wake wa Mwaka Mpya ambapo alifichua utabiri wake Jumapili iliyofuata, Januari 3 mwaka huu.
kim_2701423b

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong – Un.

“Ninaona mshale kutoka huko na utaiathiri dunia,” alisema Joshua na kuongeza, “inatubidi tuishi kwa amani kwani vita tunavyopigana nchini Syria bado vinaendelea.  Tusitake kuongeza vita vingine tena.”

Kiongozi huyo wa kidini alielezea zaidi silaha zinazoshikiliwa na taifa hilo akisema “kuna silaha huko ambazo dunia haizifahamu.  Nchi hiyo ikirusha mshale huo, dunia itakanganyikiwa.”

Siku kadhaa baadaye,  siku ya Januari 6, nchi hiyo ilitangaza kufanya jaribio “lililofanikiwa” la bomu la haidrojeni, jambo linaloongeza wasiwasi dhidi ya  nchi hiyo iliyopigwa marufuku kulimbikiza silaha za nyuklia.

Loading...

Toa comment