The House of Favourite Newspapers

NEW: Hapa Ni Korede Bello x Kelly Rowland Kwenye ‘remix’ Ya “Do Like That” – (Audio).

Korede Bello anazifuata footsteps za dada yake Tiwa Savage mdogo mdogo. Baada ya kuisogeza kwetu “Do Like That” inayosukuma views zaidi ya Millioni 10 sasa hivi kwenye YouTube staa huyo wa Nigeria kutoka Mavin Records amerudi tena, this time akiwa na mkali wa R&B kutoka Marekani Kelly Rowland pembeni.

Mara ya kwanza nausikia wimbo wa Korede Bello “Do Like That” nilijua moja kwa moja single ile itakuja kuwa hitsong kubwa sana Africa na baada ya video kuruka hewani Africa nzima ilishuhudia historia nyingine ikiandikwa na msanii huyo.

Kama haijakufikia bado basi ipokee hapa kwa mara ya kwanza, Korede Bello amerudi na remix wa wimbo wake huo akiwa amemshirikisha Kelly Rowland. Kelly Rowland alishawahi kuwa kwenye kundi moja la muziki la ‘Destiny’s Child’ pamoja na Beyonce na Michelle Williams.

Isikilize “Do Like That” remix feat. Kelly Rowalnd hapa chini.

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Comments are closed.