Kotei Afungukia usajili wake Yanga SC

KIUNGO mkabaji, James Agyekum Kotei raia wa Ghana, amefungukia tetesi za usajili wake zikimuhusisha kutua Yanga.

 

Kotei aliyeitumikia Simba kwa kipindi cha misimu mitatu kuanzia 2016, aliachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita na kutua Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu. Mghana huyo tangu atue kwenye kikosi cha Kaizer amekuwa hana maisha mazuri huku akitumia muda mwingi kuishia benchi.

 

Amedumu kwenye kikosi hicho kwa muda wa miezi sita tu, na sasa anatajwa kurudi Tanzania, huku safari hii akihusishwa na Yanga. Wakati taarifa za yeye kurudi Tanzania zikizagaa kila kona, Spoti Xtra likamtafuta na kuzungumza naye juu ya ishu hiyo.

 

Kotei ambaye aliipa Simba ubingwa wa FA mara moja na Ligi Kuu Bara mara mbili, alisema: “Taarifa hizo za mimi kurudi Tanzania si za kweli, ingawa huku Kaizer wanataka kuvunja mkataba wangu.

 

“Hiyo imekuja baada ya kocha kuleta wachezaji wapya ambao ndiyo anawatumia, huku mimi nikikosa nafasi. “Sijaambiwa chochote na wakala wangu kuhusu kujiunga na Yanga, lakini yupo bize anafanya mchakato wa mimi kwenda kucheza Ulaya. Siwezi kubaki hapa Kaizer, lazima tuvunje mkataba.”

 

Yanga katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka jana na kutarajiwa kufungwa Januari 15, mwaka huu, tayari imeshawasajili nyota watano ambao ni Ditram Nchimbi, Tariq Seif, Adeyum Saleh, Yikpe Gnamien na Haruna Niyonzima.

 

Spoti Xtra liliwatafuta viongozi wa Yanga kuzungumzia ishu hiyo, lakini hawakupatikana, lakini hivi karibuni baada ya timu hiyo kutoka sare ya mabao 2-2 na Simba, Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, alisema:

 

“Kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, tutashusha majembe mawili ya maana ili kuimarisha zaidi kikosi chetu.


Loading...

Toa comment