Kuagwa kwa King Majuto, Majonzi & Vilio Vyatawala (Picha +Video)


MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ leo Agost 9, 2018.

Mzee King Majuto alifariki dunia jana majira ya saa 2:00 usiku Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.

Baada ya kuaga mwili utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa.

Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.

 

Fuatilia tukio hilo hapa

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment