The House of Favourite Newspapers

KUAZIMWA NGUO NA LINAH, NAI ATOA POVU

Nai Kisa

BAADA ya kunangwa kwamba ameazima nguo kwa mwanamuziki, Esterlina Sanga ‘Linah’, muuza nyago kwenye video mbalimbali za wasanii wa muziki Bongo, Nai Kisa ametoa povu na kuwataka wanaomsema kufunga midomo.

Akichezesha taya na Za Motomoto News, Nai alisema hawezi kuazima nguo kwa mtu yeyote kwani ni bora arudie nguo lakini siyo kuazima, kilichotokea kwake na Linah ni kwamba nguo zimefanana ila kila mtu amenunua kwa wakati wake na ndiyo maana alifanya utani kumshukuru Linah mtandaoni kwa kumpa gauni kwa sababu yamefanana ila watu wakadhani ni kweli amemuazima.

“Hizo ni dharau sasa ina maana ndiyo nimefulia kiasi hicho mpaka nishindwe kununua gauni? Nilijua tu watu wataongea ndiyo maana nikafanya makusudi kumshukuru Linah kama amenipa ila nilifanya utani kwa sababu magauni yamefanana, yeye lake alivaa kwenye shoo Iringa mimi nimevaa kwenye bethidei ya Wolper, sasa kama kiwanda kinatoa nguo moja watu wanataka tufanyeje,” alisema Nai.

Stori: Shamuma Awadhi, Dar

Comments are closed.