The House of Favourite Newspapers

Kucha za lesi na matunda ndiyo habari ya mjini

0

Lace  NailsWiki hii nakuletea kucha mpya ambazo ndiyo habari ya mjini. Kucha hizi zinaitwa Lace  Nails, kucha za lesi lakini pia kuna Fruit Lace ‘lesi za matunda.’

Kwa wale wanaokwenda na wakati kama una nguo yako ambayo ina lesi  unaweza kutengeneza kucha za kufanana na nguo yako kama tunavyoona kwenye picha.

Jinsi ya kutengeneza.

Tengeneza kucha zako kwanza kwa kuzisafisha, baada ya hapo zichonge unavyotaka, ukimaliza chukua kipande cha lace ya rangi unayotaka inayoendana na ile uliyopaka.

Bandika juu ya kucha zako kupata shepu inayoendana na kucha yako, weka alama kisha kata na mkasi.

Baada ya hapo weka gundi kisha bandika lace yako, ukimaliza paka rangi ya kung’arisha ile nyeupe, itazidisha uimara.

Vile vile kwenye kucha ya matunda, chukua kipande kilichochorwa matunda, kata usawa wa kucha zako kisha bandika kama kawaida.

Leave A Reply