The House of Favourite Newspapers

Mr. Championi agawa zawadi

0

Mr.Championi akizidi kumwaga zawadi ya sukari kwa wasomaji wa gazeti la Championi waliokutwa wakisoma gazeti hilo eneo la kituo cha daladala cha Tegeta.

Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wasomaji wa gazeti la Championi.

Msomaji wa gazeti la Championi aliye na baiskeli akipokea zawadi ya Sukari mara tu Mr. championi kumkuta akisoma gazeti hilo eneo la Mbezi ya Tegeta.

Msomaji wa gazeti la Championin eneo la stendi ya daladala ya Goba akipokea zawadi yake kutoka kwa Mr.Championi.

Msomaji wa gazeti la Championi akionesha gazeti hilo kabla ya kupewa zawadi yake na Mr. Championi.
Mr.Championi akimkabbidhi zawadi yake ya mfuko wa sukari.
Mr.Championi akitoa zawadi kwa mwendesha bodaboda eneo la stendi ya daladala Goba mara baada ya kumkuta akisoma gazeti hilo.
Mr.Championi akiwa katika picha na msomaji wa gazeti la Championi eneo la kituo cha daladala cha Goba.
Mr.Championi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa gazeti la Championi.

Kondakta wa daladala wa eneo la stendi ya Tabata Kinyerezi akipokea zawadi yake kutoka kwa Mr.Championi mara alipomkuta na gazeti la Championi.
Mr.Championi akitoa zawadi kwa msomaji wa gazeti la Chamioni eneo la Mbezi Kimara.
Mr.Championi akiwa katika picha na msomaji wa gazeti la Championi kabla ya kupewa zawadi yake.

Wasomaji wa gazeti la Championi wakipokea zawadi kutoka kwa Mr.Championi eneo la Malamba Mawili mara baada ya kukutwa wakinunua gazeti kwa muuzaji wa magazeti.

ZIKIWA Zimebaki siku 39 kufikia Uchaguzi Mkuu wa Urais, wabunge na madiwani kama kawaida yake MR.Championi kuwajali wasomaji wake, leo alitembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kama Tegeta-Kibaoni, Goba, Mbezi Mwisho, Malamba Mawili, Kifaru, pamoja na Tabata kinyerezi kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo Sukari kwa wasomaji waliokutwa wakisoma gazeti la Championi.

Mr. Championi wakati wa utoaji zawadi hizo aliambatana na ofisa usambazaji wa Global Publishers, Yohana Mkanda, ambaye wakati Mr.Championi akigawa zawadi nae aliweza kupokea maoni mbalimbali yanayohusu magazeti ya Championi.

Aidha Mkanda aliwaahidi wasomaji wa gazeti hilo kuendelea kulisoma kwani kila Mr.Championi atakayekutwa akisoma gazeti hilo atakuwa akijipataia zawadi.“kazi kubwa ya Mr.Championi ni kuhakikisha anatoa zawadi kwa wasomaji wa gazeti la Championi sehemu yoyote atakapokutwa akisoma gazeti hilo,” alisma Mkanda.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

 

Leave A Reply