The House of Favourite Newspapers

Kufuru Maisha Ya Tiffah Sauz

DAR: KUNA watu kwenye hii dunia wamezaliwa ili waitafune! Mtoto wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Tiffah, ni miongoni mwa viumbe ambao tangu wazaliwe, maisha yao ni starehe mwanzo mwisho, Risasi Mchanganyiko limekukusanyia habari hii!

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo kilichowahi kutinga nyumbani kwa Zari Sauz, kimeeleza kuwa mtoto huyo pekee wa kike, amekuwa akipewa bata la upendeleo na mama yake kwani ndiye rafiki yake kipenzi.

“Tiffah noma, tangu amezaliwa ni bata mwanzo mwisho, angalia kuanzia mavazi ya kijanja anavyovaa kama mtu mzima, angalia viwanja anavyozunguka na mama yake wakipata chakula, yaani anakula maisha flani hivi ya juu sana,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

CHUMBA CHAKE SASA…

Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilieleza kuwa, chumba anacholala Tiffah ni cha tofauti na wanacholala watoto wengine wa Zari.

“Kitanda anacholalia Tiffah sio cha kitoto, ni kitanda haswa ambacho kwa bei ya Sauz sio chini ya milioni za Kibongo, achilia mbali yale mashuka ya gharama sana.

AWAFUNIKA MASTAA BONGO

“Wewe unafikiri kwa levo hiyo na mastaa wetu hapo Bongo wakubwa, si wengi tu watakuwa wanapigwa gepu na Tiffah. Angalia pea za viatu kwenye kabati lake, ni vya kutosha na kimoja si chini ya shilingi elfu hamsini, angalia magauni yake yalivyo mengi chumbani mwake ambayo mengi yanacheza kwenye shilingi elfu hamsini mpaka laki, usisahau anamiliki simu ya kisasa aina ya iphone ambayo gharama yake si chini ya shilingi milioni moja,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliwahi kumtembelea Zari nyumbani kwake.

KWA NINI TIFFAH ZAIDI?

Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa licha ya kuwa watoto wote watano wa Zari wanaponda raha, lakini kwa Tiffah huenda ikawa inatokana na kuwa mtoto pekee wa kike.

“Tiffah ndiye binti pekee wa Zari hivyo lazima uone kidogo kama kuna kaupendeleo fulani hivi ingawa kwa maana ya kula bata, watoto wote wa Zari hawaishi kinyonge,” kiliweka nukta chanzo hicho.

Risasi Mchanganyiko kutoka katika vyanzo mbalimbali, liliweza kufanikiwa kuzinasa picha mbalimbali zinazosadifu uhalisia wa maisha mazuri na ya gharama anayoishi binti huyo wa Zari ambaye wazazi wake waliachana Februari 14, mwaka jana.

Kuna picha zinazomuonesha akiwa kwenye hoteli za gharama akiogelea, akila vyakula ambavyo hata kwa macho tu unaona si vya vile vya ‘wenzangu na mimi’.

BABU YAKE ATOA NENO

Baada ya kumtafuta baba yake, Diamond na kutompata kwa kuwa alikuwa kwenye shoo Dubai, Falme za Kiarabu, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta babu yake, mzee Juma Abdul ‘Baba D’ ambaye alikiri kufahamu kuwa watoto hao wanakula raha zenye hadhi ya kistaa lakini akasema anatamani zaidi kama kutakuwa na maelewano ili watoto hao wawe huru kuja Bongo kwa baba yao.

“Maisha mazuri kwa wale watoto ni jambo la kawaida kwa sababu mama yao yuko vizuri, ana mashule ana maduka kule Sauz kwa hiyo hilo ni jambo la kawaida,” alisema Baba D na kuongeza: “Mimi furaha yangu labda pengine ni kuona kama wanaweza kuwa kwenye mawasiliano mazuri ili ikiwezekana, wawe wanakuja kama siyo kuishi huku kwa baba yao maana malezi ya upande mmoja wakati mwingine si mazuri sana.”

Tangu Diamond aachane na Zari, imeelezwa kuwa mawasiliano ya wawili hao si mazuri sana kiasi cha kumfanya staa huyo wa Bongo Fleva ashindwe kuwaona wanaye pindi anapohitaji kufanya hivyo.

CHUKUA HII!

Watoto watatu wa Zari; Diddy, Quincy na Pinto alizaa na marehemu mumewe Ivan Semwanga huku wengine wawili; Tiffah na Prince Nillan akizaa na Diamond.

STORI: ERICK EVARIST, RISASI

Comments are closed.